Home

MABADILIKO KUHUSU ADA YA MAOMBI YA UDAHILI
(Application fee) 

 

Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) kinapenda kuwataarifu wanafunzi wote walioomba na wanaotarajia kufanya maombi ya udahili kwa   ajili ya mwaka wa masomo 2017/2018 kwamba, ada ya kuomba udahili kwa kozi zote ni Tsh. 10,000/= kuanzia tarehe 27/7/2017. 

 

Pia tunapenda kuwataarifu wadau wote ambao tayari walikwisha lipia fomu ya udahili Kwa gharama za awali, kuwa wanatakiwa watunze kumbukumbu zao za malipo. Iwapo atachaguliwa,  fedha hiyo iliyozidi itakuwa sehemu ya ada yake, na kwa yule ambae  hatochaguliwa atarudishiwa kiasi cha fedha kinachobaki kwa utaratibu utakaokuwa umepangwa na chuo.

 

Chuo kinawakaribisha wanafunzi wote kuja kujiunga katika kozi mbalimbali zinazotolewa kuanzia katika level ya Certificate, Diploma, Degree, Postgraduate, mpaka Master. 

 

Wahi sasa  nafasi ni chache.

 

Tafadhali mara upatapo ujumbe huu mshirikishe na mwingine

 

 

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano

Chuo Kikuu cha Iringa

27/7/2017